Date: 
24-11-2016
Reading: 
Thur 24th Nov, Matthew 22:23-33 (NIV)

THURSDAY 24TH NOVEMBER 2016 MORNING                              

Matthew 22:23-33   New International Version (NIV)

Marriage at the Resurrection

23 That same day the Sadducees, who say there is no resurrection, came to him with a question. 24 “Teacher,” they said, “Moses told us that if a man dies without having children, his brother must marry the widow and raise up offspring for him. 25 Now there were seven brothers among us. The first one married and died, and since he had no children, he left his wife to his brother. 26 The same thing happened to the second and third brother, right on down to the seventh. 27 Finally, the woman died. 28 Now then, at the resurrection, whose wife will she be of the seven, since all of them were married to her?”

29 Jesus replied, “You are in error because you do not know the Scriptures or the power of God. 30 At the resurrection people will neither marry nor be given in marriage; they will be like the angels in heaven.31 But about the resurrection of the dead—have you not read what God said to you, 32 ‘I am the God of Abraham, the God of Isaac, and the God of Jacob’[a]? He is not the God of the dead but of the living.”

33 When the crowds heard this, they were astonished at his teaching.

Footnotes:

  1. Matthew 22:32 Exodus 3:6

The Sadducees did not believe in Eternal life. They asked Jesus the question by posing an unlikely example but their aim was to trick Jesus.

But Jesus pointed out that even if it was possible for a woman to marry seven brothers in succession and to outlive all of them she would not be married to any of them in heaven. Life on earth is very different from life in heaven.

Marriage is a good thing for life on earth but has no place in heaven. May God help us all to live wisely on earth and prepare for heaven.

 

ALHAMISI TAREHE 24 NOVEMBA 2016 ASUBUHI             

MATHAYO 22:23-33

23 Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza, 
24 wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao. 
25 Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake. 
26 Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba. 
27 Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye. 
28 Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye. 
29 Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu. 
30 Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni. 
31 Tena kwa habari ya kiyama ya watu, hamjalisoma neno lililonenwa na Mungu, akisema, 
32 Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. 
33 Na makutano waliposikia, walishangaa kwa mafunzo yake. 
 

Masadukayo hawakuamini kuhusu mbinguni na maisha ya milele. Kwa sababu hii walitoa mfano kumjaribu Yesu. Hata kama mfano huu unawezakuwa halisi, bado hauaathiri maisha ya Mbinguni. Maisha ya milele mbinguni ni tofauti sana na maisha hapa duniani. Ndoa ni mpango mzuri wa Mungu kwa maisha ya binadamu hapa duniani. Lakini mbinguni hatutaoa wala kuolewa.

Tuishi vizuri duniani tukijiandaa kwa maisha ya milele Mbinguni.