Date: 
26-11-2016
Reading: 
Sat 26th Nov, Isaiah 29:18-24

SATURDAY 26TH NOVEMBER 2016 MORNING                          

Isaiah 29:18-24  New International Version (NIV)

18 In that day the deaf will hear the words of the scroll,
    and out of gloom and darkness
    the eyes of the blind will see.
19 Once more the humble will rejoice in the Lord;
    the needy will rejoice in the Holy One of Israel.
20 The ruthless will vanish,
    the mockers will disappear,
    and all who have an eye for evil will be cut down—
21 those who with a word make someone out to be guilty,
    who ensnare the defender in court
    and with false testimony deprive the innocent of justice.

22 Therefore this is what the Lord, who redeemed Abraham, says to the descendants of Jacob:

“No longer will Jacob be ashamed;
    no longer will their faces grow pale.
23 When they see among them their children,
    the work of my hands,
they will keep my name holy;

    they will acknowledge the holiness of the Holy One of Jacob,
    and will stand in awe of the God of Israel.
24 Those who are wayward in spirit will gain understanding;
    those who complain will accept instruction.”

In this message from God through the prophet Isaiah there are words of encouragement. This is a message of hope to those who are disabled and who are disadvantaged in various ways. This is a message about heaven when all pains and sorrows will end.

Thank God for the comfort we receive through His word. God’s promises are reliable and trustworthy. Trust in Jesus  Christ and you will be blessed now and in eternity.   

JUMAMOSI TAREHE 26  NOVEMBA 2016 ASUBUHI                 

ISAYA 29:18-24

18 Na katika siku hiyo viziwi watasikia maneno ya hicho chuo, na macho ya vipofu yataona katika upofu na katika giza.
19 Wanyenyekevu nao wataongeza furaha yao katika Bwana, na maskini katika wanadamu watafurahi katika Mtakatifu wa Israeli. 
20 Kwa maana mwenye kutisha ameangamizwa, naye mwenye dharau amekoma, nao wote watazamiao uovu wamekatiliwa mbali; 
21 hao wamfanyao mtu kuwa amekosa katika neno, na kumtegea mtego yeye aonyaye langoni, na kumgeuza mwenye haki kwa kitu kisichofaa. 
22 Basi, Bwana aliyemkomboa Ibrahimu asema hivi, katika habari za nyumba ya Yakobo; Yakobo hatatahayarika sasa, wala uso wake hautabadilika rangi yake. 
23 Bali atakapowaona watoto wake, walio kazi ya mikono yangu, katikati yake, wao watalitakasa jina langu; naam, watamtakasa Mtakatifu wa Yakobo, nao watamcha Mungu wa Israeli. 
24 Hao nao wakosao rohoni mwao watapata kufahamu, na hao wanung'unikao watajifunza elimu.

Katika maneno haya juu Mungu  anaongea kupitia Nabii Isaya. Mungu anatoa maneno ya faraja kwa walemavu na wenye shida mbablimbali.

Watu wengi wanateseka na shida mbalimbali lakini siku mmoja Mungu atarekebisha  yote. Ni matumaini ya maisha  ya milele. Tumtumaini na tumtegemee Yesu Kristo na tutapata Baraka ya Mungu  hapa na hata milele.