Date: 
31-07-2020
Reading: 
Romans 6:15-23 (Warumi 6:15-23)

FRIDAY 31ST JULY 2020     MORNING                                                           

Romans 6:15-23 New International Version (NIV)

15 What then? Shall we sin because we are not under the law but under grace? By no means! 16 Don’t you know that when you offer yourselves to someone as obedient slaves, you are slaves of the one you obey—whether you are slaves to sin, which leads to death, or to obedience, which leads to righteousness? 17 But thanks be to God that, though you used to be slaves to sin, you have come to obey from your heart the pattern of teaching that has now claimed your allegiance. 18 You have been set free from sin and have become slaves to righteousness.

19 I am using an example from everyday life because of your human limitations. Just as you used to offer yourselves as slaves to impurity and to ever-increasing wickedness, so now offer yourselves as slaves to righteousness leading to holiness. 20 When you were slaves to sin, you were free from the control of righteousness. 21 What benefit did you reap at that time from the things you are now ashamed of? Those things result in death! 22 But now that you have been set free from sin and have become slaves of God, the benefit you reap leads to holiness, and the result is eternal life. 23 For the wages of sin is death, but the gift of God is eternal life in[b] Christ Jesus our Lord.

There are really only two masters; we are either enslaved to sin resulting in eternal death or slaves to Christ resulting in eternal life.

Now that we are in Christ, we are enslaved to Him through obedience all this is by faith. As believers, we are currently serving Him and not sin, because we cannot serve both.


IJUMAA TAREHE 31 JULAI 2020      ASUBUHI                                       

WARUMI 6:15-23

15 Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha!
16 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.
17 Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;
18 na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.
19 Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa.
20 Kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki.
21 Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti.
22 Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Katika Ulimwengu huu wapo mabwana wawili; ama tuwe watumwa wa dhambi ambayo matokeo yake ni mauti ya milele au kuwa watumwa wa Kristo ambayo karama yake ni uzima wa milele. Sasa kwa kuwa tuko ndani ya Kristo, tu watumwa wake kwa njia ya utii; na hii ni kwa imani. Sisi Wakristo tunamtumikia Yesu na siyo dhambi, kwa sababu hatuwezi kuwatumikia wote wawili.