Date: 
15-01-2021
Reading: 
Romans 6:12-14 

FRIDAY 15TH JANUARY 2021 MORNING                                                      

Romans 6:12-14 New International Version (NIV)

12 Therefore do not let sin reign in your mortal body so that you obey its evil desires. 13 Do not offer any part of yourself to sin as an instrument of wickedness, but rather offer yourselves to God as those who have been brought from death to life; and offer every part of yourself to him as an instrument of righteousness. 14 For sin shall no longer be your master, because you are not under the law, but under grace.

We must decide how we will live our lives as Christians. Making the right choice is not easy but it is possible; and certainly can be done with God’s help. When we are new in Christ after the knowledge of God and have put off the old man with his deeds, we put on the Holy Spirit with His fruit.


IJUMAA TAREHE 15 JANUARI 2021 ASUBUHI                                          

WARUMI 6:12-14

12 Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;
13 wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.
14 Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.

Tunapaswa kuamua namna ya kuishi maisha yetu kama Wakristo. Kufanya uchaguzi sahihi siyo rahisi lakini inawezekana; na hakika inaweza kufanyika kwa msaada wa Mungu. Tunapokuwa viumbe wapya ndani ya Kristo baada ya kumjua Mungu na kuuvua utu wa kale pamoja na matendo yake, tunavikwa Roho Mtakatifu pamoja na tunda lake.