MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 13 MEI, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI MUNGU HUTUSIKIA KATIKA KUOMBA KWETU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:  Wageni waliotufikia na cheti ni Familia ya Bwana Innocent Elisifa Ngowi toka usharika wa Mboni Marangu Dayosisi ya Kaskazini Kilimanjaro – Wanahamia hapa Azania Front.

3. Alhamisi ijayo tarehe 17/05/2018 kutakuwa na  maombi na maombezi yatakayoanza saa 11.00 jioni. Washarika wote mnakaribishwa.

4. Vitabu vipya vya Tumwabudu Mungu wetu vipo, vitauzwa hapo nje kwa bei ya Sh. 12,000/=.  Pia vitenge vya Kiharaka bado vipo kwa bei ya Sh. 10,000/=

5. Kuna baadhi washarika bado wanatumia bahasha zao za zamani  hivyo wanaleta usumbufu kwa wale wenye namba mpya.  Kama hukujaza fomu kwa ajili ya namba mpya usitumie bahasha yako ya zamani.   Fika ofisini ili uweze kupewa namba mpya.

6. Jumapili  ijayo tarehe  20/05/2018 katika ibada ya pili familia ya Mzee Heriel Kida watamshukuru Mungu kipekee kwa mambo mengi aliyowatendea  kwa familia yao. Zab. 138:1-5, Wimbo: TMW 319

7. Umoja wa vijana Jimbo la Kati limeandaa Ligi ya michezo ya mpira wa miguu(Football) na mpira wa pete (Netball).  Hivyo jumamosi ijayo tarehe 19/05/2018 itakuwa ni siku ya ufunguzi wa Ligi hii na kati ya Watumishi wa jimbo la kati na timu mchanganyiko ya vijana  toka sharika na mitaa ya jimbo la kati kuanzia saa 3.00 asubuhi katika viwanja  vitakavyopangwa.

8. Idara ya Theolojia, Misioni na Uinjilisti Dayosisi ya Mashariki na Pwani inapenda kuwajulisha vijana wote kuwa, kutakuwa na kongamano la vijana KKKT Taifa litakalowakutanisha vijana 1000 kutoka katika Dayosisi zote za KKKT.  Kongamano hili litafanyika tarehe 20-25/06/2018 KASSA CHARITY SCHOOL, MWANZA.  Gharama za ushiriki kwa kila kijana ni Tshs. 250,000/=.  Fomu ya kuchangia kongamano hili la vijana zimeshagawiwa kwa vijana.  Aidha kutakuwa na Kongamano la vijana Jimbo la kati litakalofanyika tarehe 03-08/07/2018 katika shule ya Kanisa Peace House Secondary – Arusha. Gharama kwa kila kila kijana mshiriki ni Tsh. 180,000/=. Vijana wote mnaombwa kushiriki, ni muhimu sana.

9. NDOA.

NDOA YA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 26/05/2018

SAA 8.00 MCHANA

Bw. Sepi Lionel Mawalla na Bi. Jestina Joseph Ngowi

Matangazo mengine ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

10. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

- Upanga: Kwa Bibi Msangi

- Kinondoni: Kwa Bibi Lwezaura

- Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Itemba

- Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi Whitsun Moshi

- Mjini kati:  Kwa Neema Meena

- Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo:Kwa Bwana na Bibi  Charles Lyimo

                                               

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.