MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 08 OKTOBA, 2017
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI UHURU WA MKRISTO
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Leo hatutakuwa na Kipindi cha maombi na maombezi, tutaungana na wenzetu kwenye semina inayoanza leo tarehe 8 hadi tarehe 15 Octoba kuanzia saa 8.00 mchana katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe itakayoongozwa na Mwalimu Christopha Mwakasege Wote mnakaribishwa.
4. Vitenge vya Miaka mia tano ya matengenezo ya Kanisa vipo. Vitauzwa hapo nje na viongozi wa Umoja wa Wanawake kwa bei ya sh. 15,000/=. Aidha Vitenge vya Kiharaka navyo bado vipo, vitauzwa hapo nje kwa bei ya shilingi elf 10. Washarika karibuni.
5. Leo tutamtolea Mungu fungu la kumi.
6. Tunapenda kuwatangazia washarika wote kuwa mafundisho ya ndoa za mwezi wa Oktoba, Novemba, Disemba Mpaka Februari 2018 yatafanyika tarehe 11 na 18 Novemba 2017 saa 3.00 asubuhi Usharika wa Magomeni Mviringo.
7. Jumanne ijayo tarehe 10/10/2017 saa 7.00 mchana kutakuwa na ibada ya ufunguzi wa Kongamano la Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani (Lutheran Wolrd Federation). Ibada itafanyika hapa Kanisa kuu Azania Front na itakuwa ni alama ya mwendelezo wa maadhimisho ya miaka 500 ya Ulutheri Duniani. Itahudhuriwa pia na Viongozi wakuu wa KKKT pamoja na Rais wa Fungamano la Makanisa ya Kulutheri Duniani na wajumbe wa Kongamano wapatao 65. Washarika wote mnakaribishwa siku hiyo.
8. Tunapenda kuwakumbusha wazazi wanaobariki watoto mwaka huu kuwa ibada itafanyika tarehe 05/11/2017 uwanja wa Taifa. Hivyo Watoto wa Kipaimara watavaa Tshirt, Sketi nyeusi na viatu vyeupe. Wavulana watavaa Tshirt, suruali nyeusi na viatu vyeusi. Tunawaomba wazazi mpeleke Sh. 15,000/= kwa Parish Worker ili Tshirt zikachukuliwe kwa pamoja. Aidha sare ya siku hiyo kwa washarika wote ni Kitenge cha miaka 500 na Tshirt. Aidha tarehe Jumamosi ijayo tarehe 14/10/2017 watoto wa Kipaimara watafanya mtihani. Wazazi muwahimize watoto.
9. Tunapenda kuwatangazia washarika kuwa Sikukuu ya Mavuno mwaka huu itafanyika tarehe 12/11/2017 katika ibada zote mbili kama kawaida. Ibada ya pili siku hiyo itaanza saa 4.00 asubuhi. Washarika tuikumbuke siku hiyo kwa maombi. Mungu awabariki.
10. NDOA
NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 28/10/2017
SAA 9.00 ALASIRI
Bw. Frank Godfrey Kanza na Bi. Eva Wynjones Kanumba
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.
11. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
a. Upanga: kwa Bwana na Bibi Happiness Nkya
b. Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale
c. Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Monyo
d. Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi T. Msangi
e. Oysterbay/Masaki: Kwa Capt. na Bibi Mkonyi
f. Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Mzee E. Kuzilwa
g. Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi Elisifa Ngowi.
h. Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Dr. na Bibi Kashilillah
Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.
RATIBA YA MAADHIMISHO YA MIAKA 500 YA MATENGENEZO YA KANISA
TAREHE |
TUKIO |
WAHUSIKA |
|
14 Oktoba 2017 |
Siku ya Kanisa na Mazingira |
Sharika/Mitaa
|
|
20 Oktoba 2017 |
Mkesha/Ubatizo wa watu wazima/kurudi kundini
|
Mbezi Beach |
|
22 Oktoba 2017 |
Ufunguzi wa Jengo la ibada Saa 2.00 asubuhi |
Usharika wa Mji mwema
|
|
28 Oktoba 2017 |
Siku ya Michezo ya pamoja. Wachungaji, Wainjilisti, P/Workers. Na Makanisa mengine kama RC, Anglikana na kada ya Watumishi
|
Viwanja vya chuo Kikuu. |
|
05 Novemba 2017 |
Kilele cha miaka 500. |
Uwanja wa Taifa. |
|
|
|||
25 Novemba 2017 |
Siku ya kanisa na Udiakonia |
|
|
02 Desemba 2017 |
Maonesho ya sanaa na Matengenezo ya Kanisa |
|
|
26 Desemba 2017 |
Ibada ya Kipaimara mwaka wa pili kwa waliochelewa (Shuleni, nk) Saa 2 asubuhi |
Azania Front Cathedral |