MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 08 OKTOBA, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI UHURU WA MKRISTO

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:  Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Leo hatutakuwa na Kipindi cha maombi na maombezi, tutaungana na wenzetu kwenye semina inayoanza leo tarehe 8 hadi tarehe 15 Octoba kuanzia saa 8.00 mchana katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe itakayoongozwa na Mwalimu Christopha Mwakasege Wote mnakaribishwa.

4. Vitenge vya Miaka mia tano ya matengenezo ya Kanisa vipo.  Vitauzwa hapo nje na viongozi wa Umoja wa Wanawake kwa bei ya sh. 15,000/=.  Aidha Vitenge vya Kiharaka navyo bado vipo, vitauzwa hapo nje kwa bei ya shilingi elf 10.  Washarika karibuni.

5. Leo  tutamtolea Mungu fungu la kumi. 

6. Tunapenda kuwatangazia washarika wote kuwa mafundisho ya ndoa za mwezi wa Oktoba, Novemba, Disemba Mpaka Februari 2018 yatafanyika tarehe 11 na 18 Novemba 2017 saa 3.00 asubuhi Usharika wa Magomeni Mviringo.

7. Jumanne ijayo tarehe 10/10/2017  saa 7.00 mchana kutakuwa na ibada ya ufunguzi wa Kongamano la Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani (Lutheran Wolrd Federation). Ibada itafanyika hapa Kanisa kuu Azania Front na itakuwa ni alama ya mwendelezo wa maadhimisho ya miaka 500 ya Ulutheri  Duniani. Itahudhuriwa pia na Viongozi wakuu wa KKKT pamoja na Rais wa Fungamano la Makanisa ya Kulutheri Duniani na wajumbe wa Kongamano wapatao 65.  Washarika wote mnakaribishwa siku hiyo.

8. Tunapenda kuwakumbusha wazazi wanaobariki watoto mwaka huu kuwa ibada itafanyika tarehe 05/11/2017 uwanja wa Taifa. Hivyo  Watoto wa Kipaimara watavaa Tshirt, Sketi nyeusi na viatu vyeupe. Wavulana watavaa Tshirt, suruali nyeusi na viatu vyeusi. Tunawaomba wazazi  mpeleke Sh. 15,000/= kwa Parish Worker ili Tshirt zikachukuliwe kwa pamoja.  Aidha sare ya siku hiyo kwa washarika wote ni Kitenge cha miaka 500 na Tshirt.  Aidha tarehe  Jumamosi ijayo tarehe 14/10/2017 watoto wa Kipaimara watafanya mtihani.  Wazazi muwahimize watoto.

9. Tunapenda kuwatangazia washarika kuwa Sikukuu ya Mavuno mwaka huu itafanyika tarehe 12/11/2017 katika ibada zote mbili kama kawaida.  Ibada ya pili siku hiyo itaanza saa 4.00 asubuhi.  Washarika tuikumbuke siku hiyo kwa maombi.  Mungu awabariki.

10. NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 28/10/2017

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Frank Godfrey Kanza  na Bi. Eva Wynjones Kanumba

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

11. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

a. Upanga: kwa Bwana na Bibi Happiness Nkya

b. Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale

c. Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Monyo

d. Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi T. Msangi

e. Oysterbay/Masaki: Kwa Capt. na Bibi Mkonyi

f. Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo:  Kwa Mzee E. Kuzilwa

g. Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi Elisifa Ngowi.

h. Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Dr. na Bibi Kashilillah

 

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.  

 

          RATIBA YA MAADHIMISHO YA MIAKA 500 YA MATENGENEZO YA KANISA

TAREHE

TUKIO

WAHUSIKA

14 Oktoba 2017

Siku ya Kanisa na Mazingira

Sharika/Mitaa

 

20 Oktoba 2017

Mkesha/Ubatizo wa watu wazima/kurudi kundini

 

Mbezi Beach

22 Oktoba 2017

Ufunguzi wa Jengo la ibada

Saa 2.00 asubuhi

Usharika wa Mji mwema

 

28 Oktoba 2017

Siku ya  Michezo ya pamoja.

Wachungaji, Wainjilisti, P/Workers. Na

Makanisa mengine kama RC, Anglikana na kada ya Watumishi

 

Viwanja vya chuo Kikuu.

05 Novemba 2017

Kilele cha miaka 500.

 Uwanja wa Taifa.

  • Ibada itakuwa moja tu Dayosisi nzima kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 7 mchana
  • Washarika wataingia kwa maandamano, wakianzia Karibu na uwanja saa 2 asubuhi.
  • Kutakuwa na ukaguzi kwa kila atakayeingia uwanjani,watu wasibebe mifuko/mifuko mingi au mikubwa, hasa wanawake (labda maji ya kunywa.

 

  • Kutakuwa na halaiki ya watoto (wanatoka baadhi ya Sharika ya Jimbo la Kusini)
  •  

25 Novemba 2017

Siku ya kanisa na Udiakonia

  •  

02 Desemba 2017

Maonesho ya sanaa na Matengenezo ya Kanisa

 

26 Desemba 2017

Ibada ya Kipaimara mwaka wa pili kwa waliochelewa (Shuleni, nk)

Saa 2  asubuhi

Azania Front Cathedral