WEDNESDAY 18TH JANUARY 2017 MORNING
Colossians 3:18-25 New International Version (NIV)
Instructions for Christian Households
18 Wives, submit yourselves to your husbands, as is fitting in the Lord.
19 Husbands, love your wives and do not be harsh with them.
20 Children, obey your parents in everything, for this pleases the Lord.
21 Fathers,[a] do not embitter your children, or they will become discouraged.
22 Slaves, obey your earthly masters in everything; and do it, not only when their eye is on you and to curry their favor, but with sincerity of heart and reverence for the Lord. 23 Whatever you do, work at it with all your heart, as working for the Lord, not for human masters, 24 since you know that you will receive an inheritance from the Lord as a reward. It is the Lord Christ you are serving. 25 Anyone who does wrong will be repaid for their wrongs, and there is no favoritism.
Footnotes:
- Colossians 3:21 Or Parents
Let us live out our Christian faith in every area of our lives. The Apostle Paul reminds us of the duties of husband, wives, parents and children so that there will be harmony in the home. Also in the workplace we need good relationships between employees and employers and colleagues. Let us all work faithfully as service to God not just to please our human employers.
JUMATANO TAREHE 18 JANUARI 2017 ASUBUHI
WAKOLOSAI 3:18-25
Wakolosai 3:18-25
18 Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.
19 Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.
20 Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana.
21 Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
22 Ninyi watumwa, watiini hao ambao kwa mwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wanadamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimcha Bwana.
23 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu,
24 mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.
25 Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo.
Tuiishi Imani yetu ya Kikristo katika maeneo yote ya maisha yetu. Sote tutekeleze wajibu wetu nyumbani na kazini. Mtume Paulo anatukumbusha wajibu wetu. Tuwe na mahusiano mazuri katika familia zetu na mahali pa kazi. Mume kwa mke tupendane na tuheshimiane na pia watoto na wazazi. Katika maeneo ya kazi waajiri na waajiriwa tushikamane vizuri ili kazi itekelezwe vema. Tuishi kikristo kila mahali na tufanye kazi yetu kwa bidii na uaminifu na kumtumikia Mungu, si binadamu tu.