Date:
06-07-2026
Reading:
Mithali 12:12-14
Jumatatu asubuhi tarehe 06.07.2026
Mithali 12:12-14
12 Asiye haki hutamani nyavu za wabaya; Bali shina lao wenye haki huleta matunda.
13 Katika kosa la midomo kuna mtego kwa mbaya; Bali mwenye haki atatoka katika taabu.
14 Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake; Na atarudishiwa matendo ya mikono yake.
Kanisa ni msingi wa malezi bora;
Tunaanza juma jipya kwa tafakari ya Mfalme Suleimani kuhusu haki. Suleimani anaandika kwamba asiye haki hutamani nyavu za wabaya, lakini shina la wenye haki huleta matunda. Suleimani anaendelea kukazia kila mmoja kutumia kinywa chake vizuri, maana kuna matokeo mema kwa kila aaminiye.
Tafakari hii ya Suleimani asubuhi ya leo inatuelekeza kuacha uovu, maana matokeo ya uovu siyo mazuri. Suleimani anahimiza kila aaminiye kuishi kwa haki ili kumzalia Mungu matunda. Kuishi kwa haki kunawezekana kwa msaada wa Mungu pekee. Basi tumtazame Kristo ili haki yake iwe kwetu, na Kanisa liendelee kuwa msingi wa malezi bora. Amina
Uwe na wiki njema
Heri Buberwa
