Date:
24-06-2026
Reading:
Yohana 17:22-23
Jumatano asubuhi tarehe 24.06.2026;
Yohana 17:22-23
22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.
23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.
Pamoja tujenge Kanisa la Bwana;
Injili ya Yohana sura ya 17 ni sala ya Yesu aliyosali, ndefu iliyoandikwa. Katika sala hii Yesu aliwaombea wanafunzi wake umoja. Somo la leo asubuhi ni sehemu ya sala hiyo, Yesu akiwaombea wanafunzi wake kuwa na umoja. Yesu anawaombea awe ndani yao, na Baba ndani yake ili wakamilike katika umoja.
Yesu alipowaombea wanafunzi wake umoja alitaka wakae kwa pamoja kama alivyowaita. Ni ujumbe unaotujia asubuhi hii kutukumbusha kukaa kwa umoja katika Kristo tukiitenda kazi yake kwa pamoja. Tupendane na kuitenda kazi ya Mungu kwa pamoja, huo ndiyo umoja katika Kristo. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
