Hii ni Pasaka;
Alhamisi asubuhi 30.04.2026
Mathayo 9:14-17
14 Wakati ule wanafunzi wake Yohana wakamwendea, wakasema, Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga, bali wanafunzi wako hawafungi?
15 Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga.
16 Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi.
17 Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.
Ndani ya Kristo tunakuwa wapya;
Wanafunzi wa Yohana walitatizwa na wao kufunga (walifunga pamoja na Mafarisayo) lakini wanafunzi wa Yesu hawakufunga! Yesu anawajibu kwamba walioalikwa harusini hawawezi kuomboleza wakati wako na bwana harusi, hakuna avaaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu, wala divai mpya haiwekwi kwenye kiriba kikuukuu.
Wanafunzi wa Yohana walifunga wakiitunza sheria, wao na Mafarisayo, wakitaka na wanafunzi wa Yesu kutunza sheria. Jibu la Yesu hapo juu linamaanisha kuwa kufunga hakukuwa na maana kumzidi Yesu waliyekuwa naye, maaana Yesu ndiye alikuwa utimilifu wa sheria. Simaanishi usifunge, bali katika kufunga huko mtazame Yesu. Yesu aliye utimilifu wa sheria ndiye hutufanya wapya daima. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
