Hii ni Pasaka;
Jumanne asubuhi tarehe 28.04.2026
Ezekieli 37:21-23
21 Ukawaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa walikokwenda, nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe;
22 nami nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi hiyo, juu ya milima ya Israeli; na mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote; wala hawatakuwa tena mataifa mawili, wala hawatagawanyikana kuwa falme mbili tena, hata milele.
23 Wala hawatajitia uchafu tena kwa vinyago vyao, wala kwa vitu vyao vichukizavyo, wala kwa makosa yao mojawapo; lakini nitawaokoa, na kuwatoa katika makao yao yote, ambayo wamefanya dhambi ndani yake, nami nitawatakasa; basi watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
Ndani ya Kristo tunakuwa wapya;
Ni unabii wa Ezekieli kuhusu kurejeshwa kwa Taifa la Israeli. Walikuwa uhamishoni, sasa Ezekieli anatabiri kurejeshwa kwao na kuwa Taifa moja. Mungu anasema kuwaweka chini ya Mfalme mmoja, kwa ahadi ya kuwaokoa na kuwatakasa kama Mungu wao daima.
Israeli wanaahidiwa kuwa chini ya ufalme wa Daudi (Eze 37:24) na Daudi anayetajwa hapa ni Yesu Kristo. Yesu Kristo anayetajwa ndiye alikuja duniani akateswa, akafa, akafufuka na kupaa mbinguni. Tukiwa ndani yake tunakuwa wapya daima. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
