Date: 
27-04-2026
Reading: 
2 Wakorintho 4:16-18

Hii ni Pasaka;

Jumatatu asubuhi tarehe 27.04.2026

2 Wakorintho 4:16-18

16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.

17 Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;

18 tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.

Ndani ya Kristo tunakuwa wapya;

Tunaanza juma lingine tukimsoma Mtume Paulo akiwaandikia watu wa Kanisa la Korintho kuishi kwa Imani. Anawaambia kwamba wakiishi katika Kristo hawalegei, japokuwa utu wa nje unachakaa, utu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Paulo anasema dhiki ya dunia ni nyepesi iliyo ya kitambo tu.

Paulo anasisitiza kuangalia visivyoonekana, maana vinavyoonekana ni vya muda tu, na visivyoonekana ni vya milele. Hapa anamaanisha imani katika Kristo ni ya milele, bali mambo tuyaonayo ni ya muda tu. Ujumbe wa Paulo kwetu asubuhi hii ni kuwa na imani katika Kristo pasipo kuchoka. Amina

Uwe na wiki njema ukiwa mpya katika Yesu Kristo 

 

Heri Buberwa 

Mlutheri