Date: 
25-04-2026
Reading: 
Isaya 55:1-5

Hii ni Pasaka;

Jumamosi asubuhi tarehe 25.04.206;

Isaya 55:1-5

1 Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila thamani.

2 Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.

3 Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.

4 Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa kabila za watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa kabila za watu.

5 Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya Bwana, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza.

Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo;

Nabii Isaya anatoa ujumbe wa faraja kwa Israeli, akiwaalika kuja kwa Bwana kujifurahisha nafsi zao kwa unono. Anawasihi kutega sikio na kumsikia Bwana akisema nao. Anawaambia kuwa Bwana Mungu wao amewatukuza, hivyo wasiwe na shaka katika maisha yao. Ulikuwa ni ujumbe wa faraja baada ya kuwa uhamishoni. 

Kufufuka kwa Yesu ni faraja kwetu kwamba tumeokolewa. Yesu alituokoa kwa kuutoa uhai wake kwa ajili yetu. Yesu huyu ndiye anatuita kumwamini na kukaa kwake, maana kwake iko faraja ya kweli, pia iko njia ya kuelekea uzima wa milele. Amina

Jumamosi njema

 

Heri Buberwa