Date: 
24-04-2026
Reading: 
Yohana 10:17-18

Hii ni Pasaka;

Ijumaa asubuhi tarehe 24.04.2026;

Yohana 10:17-18

17 Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena.

18 Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.

Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo;

Katika sura ya kumi ya Injili ya Yohana, Yesu anajitambulisha kama Mchungaji mwema. Anasema yeye ndiye mlango wa zizi, huwajua kondoo wake nao waisikia sauti yake. Mstari wa 11 ndiyo wazo la wiki hii, kwamba Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Somo linakazia Yesu kuutoa uhai kwa ajili ya kondoo wake. 

Tukiwa bado tunasherehekea kufufuka kwa Yesu, tunakumbushwa kwamba Yesu Kristo ndiye aliyeutoa uhai wake kwa ajili yetu. Kwa kufa na kufufuka kwake tumeokolewa kwa imani. Basi tuendelee kumtazama yeye aliye Mchungaji Mwema, siku zote za maisha yetu. Amina

Siku njema

Heri Buberwa