DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 19 APRILI, 2026 SIKU YA BWANA YA 2 BAADA YA PASAKA

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI:

"MCHUNGAJI MWEMA HUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YA KONDOO"

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

2. Matoleo ya Tarehe 12/04/2026

3. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake. NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174-KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA-5795794-KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 12/04/2026 ni Washarika 548

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu,inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu,Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Familia ya Bw & Bibi Victor Remmy Machange Wamebarikiwa kupata zawadi ya mtoto wa kiume tarehe 30/3/2026. Baba, Mama na mtoto wanaendelea vizuri.

8. Uongozi wa Kwaya ya Umoja unapenda kuwatangazia Wanakwaya wa vikundi vyote na washarika wanaopenda kuwa Jumanne ijayo tarehe 21/04/2026 saa 11.00 jioni kutakuwa na mazoezi ya uimbaji kwa ajili ya maandalizi ya Kantete. Mnaombwa kuhudhuria na kufika kwa wakati.

9. Jumapili ijayo tarehe 26/04/2026 tutashiriki Chakula cha Bwana. Hivyo tukumbuke kuwa siku hiyo ibada ya tatu itaanza saa 5.00 asubuhi.Washarika tujiande.

10. Baba Askofu, Dkt, Alex Gehaz Malasusa anawaalika wazee wote wa

Baraza kushiriki ibada ya shukrani itakayofanyika katika Usharika wa Mbezi Beach siku ya Jumamosi tarehe 02/05/2026 kuanzia saa 3.00asubuhi. Ibada hiyo itaongozwa na Baba Askofu mwenyewe.

11. Uongozi wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani unapenda kuwataarifu kuwa kutakuwa na semina juu ya uendeshaji wa harambee na changizo kwa ajili ya miradi na maendeleo ya Kanisa katika ngazi mbalimbali. Semina hiyo imeandaliwa na kuratibiwa na Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaa (DarTU) kwa ushirikiano wa United Evangelical Mission (UEM). Semina itafanyika tarehe 27/04/2026kuanzia saa 3.30 asubuhi hadi saa 7.30 mchana katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha DarTU Mwenge. Mnenaji Mkuu anatarajiwa kuwa Prof.Dr. Michael Vilain kutoka Ujerumani.

12. Kwaya Kuu ya Usharika itakuwa na safari ya kwenda MMorogoro tarehe 30/04/2026 mpaka tarehe 03/05/2026 kwa lengo la kufanya Mkutano Mkuu wa Kwaya. Hivyo wanaomba washarika kuwaunga mkono kwa chochote Mungu atakachowajalia ili kuungana nao kwa ajili ya maandalizi ya safari hiyo. Hivyo unaweza kuwaona viongozi wa Kwaya au Mhasibu wa Usharika. Washarika tuendelee kuiombea safari hiyo na Mkutano huo. Mungu awabariki sana

13. NDOA. NDOA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 09/05/2026

SAA 9.00 ALASIRI

  •  Bw. Fredrick Leonard Kowero na Bi. Anitha Frank Saria.

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 25/04/2026.

 NDOA HII ITAFUNGWA USHARKA WA

KKKT NKUHUNGU DODOMA MJINI KATI YA

  • Bw. Wilson Geofrey Kimaro na Bi. Doreen Godwin Rweikiza.

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

14. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Mjini kati: Kwa watashiriki hapa Kanisani saa 1.00asubuhi
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mujuni Mutembei
  • Ilala, Chang'ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
  • Oysterbay na Masaki: Kwa Bw. David na Bibi Ruth Mollel
  • Mikocheni, Kawe,Mbezi Beach: Kwa Prof. Esther Mwaikambo
  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mruma

15. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetuya Azania front.org, pia tupo Facebook na Instagram.

16. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.