DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 05 APRILI, 2026

SIKU YA BWANA YA 1 BAADA YA PASAKA

 NENO LINALOTUONGOZA NI:

“YESU KRISTO AJIDHIHIRISHA KWA WANAFUNZI WAKE”

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 5/04/2026

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 05/04/2026 ni Washarika 935 na Jumatatu ya Pasaka ni 246

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Uongozi wa Usharika pamoja na Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii unapenda kumshukuru Mungu sana kwa ibada nzuri ya Wazee iliyofanyika Jana jumamosi tarehe 11/04/2026 ambayo iliambatana na Meza ya Bwana. Mungu awabariki wote walioweza kuhudhuria ibada hiyo.

8. Leo tarehe 12/04/2026 tutampongeza Mch. Charles Mzinga pamoja na familia yake kwa kipindi alichotumika hapa Kanisa Kuu Azania Front.

9. SHUKRANI. JUMAPILI IJAYO TAREHE 19/04/2026 KATIKA IBADA YA TATU SAA 4.30 ASUBUHI

  •  Mzee wetu wa Kanisa Mama Rebecca Mwangoka atamshukuru Mungu kwa mema mengi, kumvusha salama katika afya, majaribu mengi, kuwatetea watoto wake katika maisha yao pamoja na kumuepusha na wezi ambao waliruka geit na kupigwa upofu hawakuona kitu.

Neno: Zaburi 23:1-6, TMW 391

10. NDOA.

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 25/04/2026. NDOA IFUATAYO ITAFUNGWA USHARKA WA KKKT NKUHUNGU DODOMA MJINI KATI YA

  •  Bw. Wilson Geofrey Kimaro na Bi. Doreen Godwin Rweikiza.

 KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 19/04/2026

 SAA 7.00 MCHANA

 Bw. Mringi Petro Ndesanjo na Bi. Upendo Jailos Makundi

 Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Mjini kati: Kwa watashiriki hapa Kanisani saa 1.00 asubuhi

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mcharo Mlaki

- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Zimba

12. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

13. Zamu: Zamu za wazee ni Wazee wote

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.