Hii ni Pasaka;
Alhamisi asubuhi tarehe 09.04.2026
Matendo ya Mitume 13:32-37
32 Na sisi tunawahubiri habari njema ya ahadi ile waliyopewa mababa,
33 ya kwamba Mungu amewatimizia watoto wetu ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu; kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili, Wewe ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa.
34 Tena ya kuwa alimfufua katika wafu, asipate kurudia uharibifu, amenena hivi, Nitawapa ninyi mambo matakatifu ya Daudi yaliyo amini.
35 Kwa hiyo anena na pengine, Hutamwachia Mtakatifu wako kuona uharibifu,
36 Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.
37 Bali huyu aliyefufuliwa na Mungu hakuona uharibifu.
Yesu mfufuka kaa pamoja nasi
Paulo yuko na Barnaba anahubiri hekaluni, akirejea wokovu kwa Taifa la Mungu kwa njia ya kifo na ufufuko wa Yesu Kristo. Anasema baba zao (Israeli) waliahidiwa ukombozi, sasa Paulo anasema habari za ukombozi huo ndizo wanazihubiri. Paulo anasema Mungu aliitimiza ahadi ya wokovu kwa kumfufua Yesu Kristo, na Kristo huyu ni mkuu kuliko Daudi.
Paulo na Barnaba walinena kwa ushujaa habari za wokovu kwa njia ya kifo cha Yesu. Ni wito kwetu kuwa na uhakika wa wokovu, kwamba kwa kifo chake Yesu na kufufuka kwake tumeokolewa. Kufufuka kwa Yesu kutukumbushe kuwa wokovu wetu hauna shaka, hivyo tumpe mioyo yetu aitawale na kutupa uzima wa milele. Amina
Alhamisi njema
Heri Buberwa
