DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 05 APRILI, 2026
SIKU YA KUKUMBUKA KUFUFUKA KWA YESU KRISTO (PASAKA)
NENO LINALOTUONGOZA NI:
“UFUFUKO WA YESU NI LIMBUKO LA WALIO HAI”
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 29/03/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 29/03/2026 ni Washarika 820 na Sunday School 263. Alhamisi kuu 466, Ijumaa Kuu 1,285
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Kesho jumatatu tarehe 06/04/2026 saa 2.00 asubuhi kutakuwa na ibada moja ambayo itaambatana na Ubatizo. Kwaya zote zitahudumu. Wazee wote watakuwa zamu.
8. Leo tarehe 05/04/2026 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.
9. Uongozi wa Kwaya ya Umoja unapenda kuwatangazia wanakwaya wote kuwa Alhamisi ijayo tarehe 09/04/2026 kutakuwa na mazoezi ya Kwaya Umoja kwa ajili ya kufanya maandalizi ya nyimbo za jumapili kumpongeza Mch. Mzinga.
10. Jumamosi ijayo tarehe 11/04/2026 kutakuwa na ibada ya wazee kuanzia miaka 65 ambayo itaambatana na Meza ya Bwana. Ibada hii itafanyika saa 3.00 asubuhi. Wazee wote wanaombwa kujiandaa kuhudhuria ibada hiyo. Mungu awabariki
11. Jumapili ijayo tarehe 12/04/2026 Kutakuwa na ibada moja tu ambayo itaanza saa 2.00 asubuhi ili kupata nafasi nzuri ya kumpongeza Mch. Charles Mzinga pamoja na familia yake kwa kipindi alichotumika hapa Kanisa Kuu Azania Front. Jumuiya zote, Vikundi vyote na Washarika wote mnaombwa kujiandaa kwa ajili ya siku hiyo. Mungu awabariki.
12. SHUKRANI. JUMAPILI IJAYO TAREHE 12/04/2026
- Familia ya Prof. na Bibi Saitiel M. Kulaba watamshukuru Mungu kwa Prof. Kulaba kutimiza miaka 80, Miaka 20 tangu astaafu, Kumtunza na kumponya toka akiwa kijana baada ya kuumwa na nyoka mwaka 1976 pamoja na kunusurika kugongwana gari baada ya kuteleza kwenye barabara yenye barafu akiwa University College London 1997.
Neno: Zaburi 103:1-5, Wimbo: TMW 51
13. NDOA.
KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 19/04/2026
SAA 7.00 MCHANA
Bw. Mringi Petro Ndesanjo na Bi. Upendo Jailos Makundi
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 11/04/2026. NDOA IFUATAYO ITAFUNGWA USHARKA WA KKKT BOKO SAA 9. ALASIRI KATI YA
-
Bw. Benjamin Magelan Sakinoi na Bi. Anastazia Thomas Kashililah
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
14. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Mjini kati: Kwa watashiriki hapa Kanisani saa 1.00 asubuhi
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
- Kinondoni: Kwa ………………….
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bi. Elyfrida Njowoka Edwin
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa……………
- Oysterbay na Masaki: Kwa……………
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa……………
- Upanga: Kwa……………
15. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
16. Zamu za wazee ni Kundi la Pili
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
