DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA

 TAREHE 29 MACHI, 2026

SIKU YA BWANA YA MWISHO KABLA YA PASAKA

(PALMARUM-SIKU YA MITENDE)

 NENO LINALOTUONGOZA NI:

“NDIYE MBARIKIWA AJAYE KWA JINA LA BWANA”

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 22/03/2026

Jumla - Tshs 22,787,500/= +USD 9,153/=+SA RAND 10,+DIRHAM 5

MATOLEO KATIKATI YA WIKI

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 15/03/2026 ni Washarika 831 na Sunday School 224

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia wazazi kuwa wanafunzi ambao hawakufanya mtihani wa Dayosisi wa kuingia mwaka wa pili wanapaswa kufanya mtihani huo siku ya jumanne tarehe 31/03/2026 saa 4.00 asubuhi pamoja na wale waliopata alama chini ya 50 hamsini nao watarudia kufanya mtihani huo.

8. Jumatano ijayo tarehe 01/04/2026 saa 11.00 jioni tutaendelea na ibada ya Kwaresma. Kwaya zote zitahudumu. Wazee wote watakuwa zamu.

9. Jumapili ijayo tarehe 05/04/2026 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.

10. Jumamosi ya tarehe 11/04/2026 kutakuwa na ibada ya wazee kuanzia miaka 65 ambayo itaambatana na Meza ya Bwana. Ibada hii itafanyika saa 3.00 asubuhi. Wazee wote wanaombwa kujiandaa kuhudhuria ibada hiyo. Wale ambao watakuwa na changamoto ya usafiri taarifa ifike ofisi ya Mchungaji ili waweze kuwezeshwa kufika katika ibada hiyo. Washarika tuendelee kuiombea ibada hiyo.

11. Jumapili ya tarehe 12/04/2026 katika ibada zote tatu tutampongeza Mch. Charles Mzinga pamoja na familia yake kwa kipindi alichotumika hapa Kanisa Kuu Azania Front. Jumuiya zote, Vikundi vyote na Washarika wote mnaombwa kujiandaa kwa ajili ya siku hiyo. Mungu awabariki.

12. NDOA. KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 19/04/2026

 SAA 7.00 MCHANA

 Bw. Mringi Petro Ndesanjo na Bi. Upendo Jailos Makundi

 Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

13. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Mjini kati: Kwa watashiriki hapa Kanisani saa 1.00 asubuhi

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo

- Kinondoni: Kwa Prof. Geofrey Mmari

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Christopha Kivulenge

- Ilala, Chang’ombe, Buguruni:, Oysterbay na Masaki:, Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach:, Upanga: Watashiriki ibada hapa Kanisani

14. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

15. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza

 

16. RATIBA YA PASAKA

ALHAMISI Tarehe 02/04/2026

Zitakuwepo ibada 2

IBADA YA KINGEREZA saa 11: jioni

IBADA YA KISWAHILI saa 1:00 usiku

 

IJUMAA KUU tarehe 03/04/2026

Zitakuwepo ibada 3 

IBADA YA KWANZA - KISWAHILI

SAA 2.00 ASUBUHI

IBADA YA PILI - KINGEREZA SAA 4.30 ASUBUHI

IBADA YA TATU – KISWAHILI SAA 8:00 MCHANA

ITAAMBATANA NA IGIZO LA PASAKA  

JUMAPILI YA PASAKA tarehe 05/04/2026

ZITAKUWEPO IBADA TATU KAMA KAWAIDA

IBADA YA KWANZA – KISWAHILI SAA 1:00 ASUBUHI

IBADA YA PILI – KINGEREZA SAA 3:00 ASUBUHI

IBADA YA TATU - KISWAHILI SAA 4:30 ASUBUHI

 

JUMATATU TAREHE06/04/2026

ITAKUWEPO IBADA MOJA SAA 2:00 ASUBUHI 

ITAAMBATANA NA UBATIZO