DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 08 MACHI, 2026
SIKU YA BWANA YA 4 KABLA YA PASAKA
NENO LINALOTUONGOZA SIKU NI
MAZINGIRA NI UHAI TUYATUNZE
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 01/03/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
5. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
6. Jumatano ijayo tarehe 11/03/2026 saa 11.00 jioni tutaendelea na ibada ya Kwaresma. Siku hiyo Wanawake wataongoza ibada kurudia Kitabu cha maombi ya Dunia. Sare ni Kitenge chetu kipya cha Kiharaka. Kwaya zote zitahudumu. Wazee wote watakuwa zamu wakishirikiana na Wanawake.
7. Jumapili ijyao tarehe 15/03/2026 ni siku ya ubatizo wa watoto na kurudi kundini. Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.
8. SHUKRANI: Jumapili ijayo tarehe 15/03/2026 familia mbili zitamshukuru Mungu.
Ibada ya Kwanza saa 1.00 asubuhi
- Familia ya Janet watamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowatendea katika maisha yao ikiwa ni pamoja na Janet kukumbuka siku yake ya kuzaliwa tarehe 15/03, afya na ulinzi.
Neno: Isaya 12:45, Wimbo: TMW 319 Yesu unipendaye
Ibada ya Tatu saa 4.30 asubuhi
- Familia ya Bibi Anna Kaduri inapenda kumshukuru Mungu kwa kuwatia nguvu na kuwawezesha kumuuguza Baba Allen Kaduri hadi alipomaliza safari yake hapa duniani.
- Neno: 2 Wakoritho 1:3-4, Wimbo: Kwaya ya wanawake
9. Jumamosi ya tarehe 11/04/2026 kutakuwa na ibada ya wazee kuanzia miaka 65 ambayo itaambatana na Meza ya Bwana. Wazee wote wanaombwa kujiandaa kuhudhuria ibada hiyo. Wale ambao watakuwa na changamoto ya usafiri wafike ofisi ya Mchungaji ili waweze kuwezeshwa kufika katika ibada hiyo. Washarika tuendelee kuiombea ibada hiyo.
10. Jumapili ya tarehe 12/04/2026 katika ibada zote tatu tutampongeza Mch. Charles Mzinga pamoja na familia yake kwa kipindi alichotumika hapa Kanisa Kuu Azania Front. Jumuiya zote, Vikundi vyote na Washarika wote mnaombwa kujiandaa kwa ajili ya siku hiyo. Mungu awabariki.
11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Happiness Nkya
- Mjini kati: Kwa Dr. Naomi
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Korosso
- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Dr. na Bibi David Ruhago
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni:, Oysterbay na Masaki:, Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach:, Watashiriki ibada hapa Kanisani
12. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
13. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili Watashirikiana na Wanawake.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
