Ijumaa asubuhi tarehe 28.11.2025
Mathayo 22:23-33
23 Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza,
24 wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao.
25 Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake.
26 Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba.
27 Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.
28 Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye.
29 Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.
30 Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni.
31 Tena kwa habari ya kiyama ya watu, hamjalisoma neno lililonenwa na Mungu, akisema,
32 Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai.
33 Na makutano waliposikia, walishangaa kwa mafunzo yake.
Uzima wa milele upo kwa ajili yako;
Masadukayo walikataa kuwepo kwa ufufuo wa wafu na maisha yajayo baada ya ulimwengu huu. Waliamini kuwa roho ikiachana na mwili ndiyo mwisho. Katika somo la leo wanamuuliza Yesu kuhusu maisha baada ya kifo kwa mwanamke aliyeolewa na ndugu saba bila kupata mtoto. Bila shaka walitaka kumsikia Yesu kuhusu maisha yajayo ambayo waliyapinga.
Yesu akijua mawazo yao, alitumia mfano wao kuwajibu, kwamba huko hakuna kuoa wala kuolewa. Yesu alitaka wawaze juu ya maisha yajayo kwa msingi wa imani katika yeye. Yesu anawaambia kuwa Yeye ndiye Mungu wa Isaka na Yakobo, Mungu wa walio hai. Yesu alikuwa anataka waamini kwamba upo uzima wa milele katika yeye, na siyo vinginevyo. Uzima wa milele upo kwa ajili yetu kwa njia ya Yesu Kristo. Amina
Ijumaa njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650
