Jumatatu asubuhi tarehe 17.11.2025
Mathayo 24:36-41
36 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,
39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
40 Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;
41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.
Jiandae kwa hukumu ya mwisho;
Yesu anafundisha kuhusu kurudi kwake, akisema siku ile hakuna aijuaye hata malaika walioko mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake. Yesu anasema kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu, ndivyo itakavyokuwa kurudi kwake. Yaani watu walidharau kitendo cha Nuhu kutengeneza safina, gharika iliposhuka wakaangamia wote! Hapa kulikuwa na fundisho la kutodharau neno la Mungu.
Jambo la muhimu tunaloliona Jumatatu ya leo ni kujiandaa kwa hukumu ya mwisho. Hukumu ya Mungu haina upendeleo, ni ya haki. Wakili wako ni maisha yako, hivyo sikiliza Injili uamue na kutenda ipasavyo. Tutimize wajibu wetu kwa kumfuata Kristo ili tusije kuangamia kama watu wa wakati ule wa Nuhu. Jiandae kwa hukumu ya mwisho. Amina
Uwe na wiki njema ukitafakari juu ya hukumu ya mwisho.
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650
