Date: 
12-11-2025
Reading: 
Yoeli 3:6-9

Jumatano asubuhi tarehe 12.11.2025

Yoeli 3:9-16

9 Tangazeni haya kati ya mataifa; takaseni vita; waamsheni mashujaa; watu wa vita na wakaribie; na wapande juu.

10 Yafueni majembe yenu yawe panga, na miundu yenu iwe mikuki; aliye dhaifu na aseme, Mimi ni hodari.

11 Fanyeni haraka, mje, enyi mataifa yote, wa pande zote, jikusanyeni pamoja; na huko watelemshe mashujaa wako wote, Ee Bwana.

12 Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafau; maana huko ndiko nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote.

13 Haya! Utieni mundu, maana mavuno yameiva; njoni, kanyageni; kwa maana shinikizo limejaa, mapipa nayo yanafurika; kwani uovu wao ni mwingi sana.

14 Makutano makubwa, makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku ya Bwana i karibu, katika bonde la kukata maneno.

15 Jua na mwezi vimetiwa giza, na nyota zimeacha kuangaza.

16 Naye Bwana atanguruma toka Sayuni, atatoa sauti yake toka Yerusalemu; na mbingu na nchi zitatetemeka; lakini Bwana atakuwa kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli.

Tuvumilie hata mwisho katika Bwana;

Sura ya tatu ya unabii wa Yoeli inahusu hukumu ya mwisho kwa mataifa yote na ukombozi wa watu wa Mungu. Inaonesha jinsi Mungu atakavyowakusanya mataifa yote katika bonde la Yehoshafati kuhukumiwa kwa kutenda uovu. Sura inaisha kwa baraka zijazo kutoka kwa Bwana, kupewa nchi, maji yaliyo hai na ushindi kwa wateule wa Mungu.

Somo letu ni sehemu ya maudhui hayo, ambapo Bwana anawaita watu kukusanyika pamoja, tayari kwa hukumu. Yoeli anasema Bwana atanguruma toka Sayuni, mbingu zitatetemeka, lakini Bwana ndiye atakuwa kimbilio la watu wake. Hapa Bwana alikuwa anawakumbusha watu wake kwamba ipo hukumu. Ni kweli, hujumu inakuja. Tutaiepuka tukivumilia hata mwisho katika Bwana. Amina

Jumatano njema 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com