Date: 
05-11-2025
Reading: 
Mathayo 5:13

Jumatano asubuhi tarehe 05.11.2025

Mathayo 5:13

Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.

Tunaitwa kuwa wenyeji wa mbinguni;

Leo asubuhi tunasoma sehemu ya hotuba ya Yesu mlimani akifundisha juu ya yampasayo kila aaminiye ili kuingia katika Ufalme wa Mungu. Tunaona Yesu akifundisha umati uliomsikiliza kwamba wao ni chumvi ya dunia. Lakini anawauliza, chumvi ikiharibika itatiwa nini ikolee? Haifai tena kabisa, labda kutupwa nje na kukanyagwa na watu. 

Sote tunafahamu kuwa chakula bila chumvi hakina utamu, na wengi wetu tunatumia chumvi labda wale wachache kwa ushauri wa daktari. Ukristo usio na ushuhuda ni sawa na chumvi iliyoharibika, haifai. Yesu alikuwa anawaambia waliomsikiliza kuwa wafuasi wa kweli. Mawazo, maneno na matendo yetu yawe halisi katika Kristo, vinginevyo ukristo wetu utakuwa haufai. Amina

Jumatano njema 

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com