Date: 
29-10-2025
Reading: 
Marko 11:15-18

Jumatano asubuhi tarehe 29.10.2025

Marko 11:15-18

15 Wakafika Yerusalemu, naye akaingia ndani ya hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao wauzao njiwa;

16 wala hakuacha mtu achukue chombo kati ya hekalu.

17 Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.

18 Wakuu wa makuhani na waandishi wakapata habari wakatafuta jinsi ya kumwangamiza; maana walimwogopa, kwa sababu mkutano wote walishangaa kwa mafundisho yake.

Ushuhuda wetu;

Ondoa yaliyo chukizo mbele za Mungu;

Ilikuwa kawaida ya watu kwenda hekaluni na vitu vya kuuza kama kazi za mikono, mazao ya shamba n.k kwa ajili ya kubadilishana na fedha ili kutoa sadaka. Mnada tunaofanya leo baada ya ibada nje haujaanza leo. Ilifanyika hivyo kwa sababu baadhi ya watu hawakuwa na fedha taslimu. Sasa ilifikia hatua ikawa eneo la biashara, zikaanza kupangwa meza kufanya biashara, hekalu likawa genge!

Ndipo tunaona Yesu akiingia hekaluni na kupindua meza zao wote wabadili fedha na viti vya wauzao njiwa. Aliwafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu. Akawaambia nyumba yangu ni nyumba ya sala, nyie mnaifanya pango la wanyang'anyi? Waandishi na makuhani wakatafuta kumwangamiza, maana alikuwa tishio kwa mafundisho yake. Yesu anaposafisha hekalu akisema ni nyumba ya sala, anatukumbusha kuwa wasafi wa roho zetu tukimwamini na kumcha yeye siku zote za maisha yetu. Amina

Jumatano njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com