Date: 
23-10-2025
Reading: 
Marko 4:35-41

Alhamisi asubuhi tarehe 23.10.2025

Marko 4:35-41

35 Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo.

36 Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.

37 Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji.

38 Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?

39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.

40 Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?

41 Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?

Imani Iletayo ushindi;

Yesu anauacha mkutano na kuvuka kuelekea ng'ambo akiwa na wanafunzi wake. Wakiwa baharini ikatokea dhoruba kuu ya upepo, chombo kikapigwa na mawimbi na kikaanza kujaa maji. Yesu alikuwa amelala, wanafunzi wakamwamsha wakisema Mwalimu tuokoe tunaangamia. Yesu akaamka na kuukemea upepo, akaiambia bahari nyamaza utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu. 

Yesu anawauliza wanafunzi wake kwa nini walikuwa waoga? Anawauliza kwamba bado hamna imani? Wanafunzi wakajawa na hofu wakishangaa Yesu ni nani hadi pepo na bahari vinamtii! Bila shaka wanafunzi hawakuwa na imani ndiyo maana waliingiwa hofu. Tusiwe na hofu, bali tujawe na imani katika Yesu Kristo. Amina

Alhamisi njema 

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com