Date: 
17-10-2025
Reading: 
Kutoka 2:16-20

Ijumaa asubuhi tarehe 17.10.2025

Kutoka 2:16-20

16 Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao.

17 Wachungaji wakaja wakawafukuza; lakini Musa akasimama, akawasaidia, akalinywesha kundi lao.

18 Walipofika kwa Reueli baba yao, akasema, Imekuwaje hata mkarejea mapema leo?

19 Wakasema, Mmisri mmoja alituokoa katika mikono ya wachungaji, tena zaidi ya hayo, akatutekea maji, akalinywesha kundi.

20 Akawaambia binti zake, Yuko wapi basi? Mbona mmemwacha mtu huyo? Mwiteni, ale chakula.

Kristo ametuweka huru;

Baada ya Yusufu kufa, Israeli waliishi maishi magumu sana ya utumwa ndani ya Misri. Nguvu yao ilihofiwa, hivyo iliamriwa watoto wa kiume wakizaliwa wauawe, japokuwa wakunga hawakulitekeleza hili. Musa alizaliwa akatupwa mtoni akaokotwa na binti Farao. Siku moja Musa akiwa amekua, akaona Mmisri akimwonea Mwebrania, akampiga yule Mmisri akamuua na kumfukia mchangani. 

Siku nyingine akawaona Waebrania wawili wakigombana. Musa akamuuliza yule aliyemuonea mwenzake mbona unamdhulumu mwenzio? Yule aliyekuwa anamdhulumu akamuuliza Musa, kwamba tangu lini umekuwa Mkuu wetu Waebrania? Unataka kuniua kama yule Mmisri? Musa ndipo akashtuka na kujua kwamba jambo lile lilifahamika. Farao alipata habari zote hizi, akapanga kumuua Musa. Lakini Musa akakimbia na kuelekea Midiani.

Ndipo somo linapoanzia hapo;

Musa akiwa yuko ukimbizini anawasaidia binti saba wa kuhani kunywesha mifugo ya baba yao, maana wachungaji walikuwa na tabia ya kuwafukuza. Siku hiyo wakanywesha mifugo yao kwa urahisi na kurudi nyumbani mapema. Walipofika wakamsimulia baba yao jinsi Musa alivyowasaidia kunywesha mifugo na kurudi nyumbani mapema. Ukiendelea kusoma unaona kuhani yule akimpa mke Musa. Mungu alikuwa akimtunza Musa kwa ajili ya kazi ya kuwaongoza Israeli kutoka Misri. Nasi Bwana ametuita kumtumikia, tuwe tayari kwa wakati ufaao na usiofaa. Amina

Ijumaa njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com