Alhamisi asubuhi tarehe 16.10.2025
Matendo ya Mitume 16:6-12
6 Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia.
7 Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa,
8 wakapita Misia wakatelemkia Troa.
9 Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie.
10 Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.
11 Basi tukang'oa nanga kutoka Troa, tukafika Samothrake kwa tanga moja, na siku ya pili tukafika Neapoli;
12 na kutoka hapo tukafika Filipi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha.
Kristo ametuweka huru;
Paulo alikuwa ameungana na Sila, walipojaribu kwenda Bithinia Roho Mtakatifu hakuwaruhusu. Wakaenda Tora, Paulo alitokewa na maono usiku kuelekea Makedonia. Huko aliona Mungu amewaita kwenda kuhubiri. Wakatoka kuelekea Makedonia na hatimaye wakafika Filipi, mjini Makedonia ambao ulikuwa mji mkuu katika jimbo lile. Walikaa hapo siku kadha wa kadha.
Somo linaonesha Paulo na Sila wakikatazwa kwenda Bithinia, lakini Roho wa Mungu anawaelekeza kuelekea Makedonia. Paulo na Sila waliongozwa na Mungu katika utume wao. Ndiyo maana hawakuelekea Bithinia, wakaelekea Makedonia. Inatukumbusha kumwamini Yesu Kristo na kumfanya kiongozi wetu, siku zote za maisha yetu. Amina
Siku njema.
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650