Jumanne asubuhi tarehe 07.10.2025
Mathayo 15:32-39
32 Yesu akawaita wanafunzi wake, akasema, Nawahurumia mkutano, kwa kuwa yapata siku tatu wamekaa pamoja nami, wala hawana kitu cha kula, tena kuwaaga wakifunga sipendi, wasije wakazimia njiani.
33 Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hata kushibisha mkutano mkuu namna hii?
34 Yesu akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, na visamaki vichache.
35 Akawaagiza mkutano waketi chini;
36 akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.
37 Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate makanda saba, yamejaa.
38 Nao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila wanawake na watoto.
39 Akawaaga makutano, akapanda chomboni, akaenda pande za Magadani.
Mungu hututunza kwa uwezo wake mkuu;
Yesu aliwaita wanafunzi wake akawaambia kuwapa mkutano chakula. Alikuwa amekaa na watu kwa siku tatu, hivyo aliwahurumia maana hawakuwa na chakula. Wanafunzi wakaonesha kuwa hawakuwa na chakula, lakini Yesu akawataka kuwapa walicho nacho, mikate saba na visamaki vichache. Yesu aliagiza watu wakae chini, akabariki ile mikate saba na samaki. Watu elfu nne wakala na kusaza (hao ni bila wanawake na watoto).
Wanafunzi wakiwa wanawaza kwamba pale wasingepata chakula cha kuwapa watu, Yesu anawaambia kuwapa chakula,walichokuwa nacho. Huruma yake ilikuwa juu ya umati uliomsikiliza kwa siku tatu mfululizo. Huruma ya Yesu iko kwetu hata sasa, maana yeye hututunza kwa uwezo wake mkuu. Mwamini sasa uokolewe. Amina
Jumanne njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650