Date: 
04-10-2025
Reading: 
Waamuzi 13:24-25

Jumamosi asubuhi tarehe 04.10.2025

Waamuzi 13:24-25

24 Basi yule mwanamke akamzaa mtoto mwanamume akamwita jina lake Samsoni, mtoto huyu akakua, Bwana akambarikia.

25 Roho ya Bwana ikaanza kumtaharakisha katika Mahane-dani, katikati ya Sora na Eshtaoli.

Tuwapende na kuwajali watoto katika Bwana; 

Somo la asubuhi hii ni sehemu ya mwanzo wa historia ya Samsoni. Ukianzia kusoma mstari wa kwanza, mke wa Manoa ambaye alikuja kuwa mama yake Samsoni alitokewa na Malaika akapewa habari njema kuwa atachukua mimba na atazaa mtoto mwanamume. Bila shaka ilikuwa habari njema na ya furaha sana maana mwanamke yule alikuwa tasa. Malaika alimwambia yule mwanamke kwamba mtoto huyo angekuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni mwa mama yake hata siku ya kufa kwake.

Ukiendelea kusoma unaona tangazo la kuzaliwa kwa mtoto mwanamume likipokelewa, na somo la leo ndiyo tukio lenyewe, kwamba mtoto anazaliwa na kuitwa Samsoni. Leo hatumuongelei Samsoni na yaliyotokea kuhusu yeye, bali Manoa na mke wake waliomtegemea Mungu akawapa mtoto katika hali ya utasa. Na zaidi, mtoto ambaye alikuwa mnadhiri wa Mungu. Watoto tulio nao ni zawadi toka kwa Mungu. Hivyo tumshukuru kwa zawadi hii ya watoto, na tuwafundishe kumjua yeye aliye njia ya kweli na uzima. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com