Date: 
03-10-2025
Reading: 
Mithali 19:8

Ijumaa asubuhi tarehe 03.10.2025

Mithali 19:18

Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.

Tuwapende na kuwajali watoto katika Bwana;

Asubuhi ya leo tunasoma juu ya kumrudi mtoto, maana katika kumrudi kuna tumaini. Suleimani anaandika kumrudi mtoto akimaanisha kufuatilia mwenendo wake na kumuonya, kumsahihisha, kumuelekeza jinsi apashwavyo kutenda katika maisha ya kila siku. Suleimani anasema usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake, yaani usimuone mtoto anapotea ukanyamaza. 

Asubuhi hii tukumbushane wajibu wetu kila mmoja;

-Tunawarudi watoto wetu? 

-Tunawakosoa wanapokosea?

-Tunawaelekeza kubaki katika njia sahihi?

Liko tumaini katika kuwarudi watoto wetu, basi tusikaze nafsi zetu wakati watoto wetu wanaangamia. Shetani yuko mlangoni, tuwaongoze kumuepuka huyo shetani kwa kuwaelekeza njia ya Kristo. Amina

Ijumaa njema 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com