Date: 
29-08-2025
Reading: 
Wagalatia 6:6-10

Ijumaa asubuhi tarehe 29.08.2025

Wagalatia 6:6-10

6 Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote.

7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.

9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.

10 Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.

 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.

9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.

10 Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.

Haki huinua Taifa;

Ni sura ya mwisho ya waraka wa Mtume Paulo kwa Wagalatia, ambapo ujumbe wake ni watu kuishi kwa pamoja wakirejezana kwa upole katika safari ya imani. Ni wito wa kuchukuliana mizigo, kila mmoja akimtendea mwenzake wema. Katika kutenda yote, Paulo anakazia kwamba wasidanganyike, maana chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna. Paulo anasema apandaye kwa mwili atavuna uharibifu, na apandaye kwa Roho atavuna uzima wa milele.

Anachosema Paulo ni matumizi bora ya wakati kwa kuwepo kwetu duniani tukitenda yatupasayo, yaani kila aaminiye kuishi akitenda kwa Utukufu wa Mungu. Paulo anahitimisha kwamba tusichoke katika kutenda mema maana tutavuna kwa wakati wake tusipozimia Roho, yaani tusiiache imani yetu maana ni njia ya kuurithi uzima wa milele. Amina

Ijumaa njema

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com