Date:
27-08-2025
Reading:
Mathayo 27:24-25
Jumatano asubuhi tarehe 27.08.2025
Mathayo 27:24-25
24 Basi Pilato alipoona ya kuwa hafai lo lote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe.
25 Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu.
Haki huinua Taifa;
Yesu alipelekwa mbele ya Pilato kushtakiwa ili ipatikane sababu ya kumuua, lakini somo la leo asubuhi linaonesha Pilato akimuona Yesu bila hatia. Kwa lugha ya sasa naweza kusema alitaka kumuachia huru, ndiyo maana alinawa mikono mbele ya washtaki wa Yesu akisema yeye (Pilato) hana hatia kwa mtu mwenye haki (Yesu) akawaambia waangalie hilo jambo wenyewe.
Kwanza, Pilato anamtaja Yesu kama mwenye haki (24). Pili, Pilato analazimishwa na nguvu ya umma kumsulibisha Yesu (25). Umma ulisema damu yake (Yesu) iwe juu yetu na juu ya watoto wetu. Tuache kutenda mambo kwa kufurahisha nafsi zetu wakati wengine wakiumia. Huo ni ukatili, siyo haki. Ujumbe wangu kwako asubuhi hii;
1. Usiwe kama Pilato aliyeshindwa kutumia nafasi yake kama kiongozi, akalazimishwa na nguvu ya umma kumsulibisha Yesu. Tumia nafasi yako kutenda haki
2. Nguvu ya umma itumike vizuri katika jamii yetu. Swala lisiwe nguvu ya umma, bali nguvu ya umma katika nini, kwa Utukufu wa Mungu.
Siku njema. Amina
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650