Date: 
26-08-2025
Reading: 
Zaburi 37:32-34

Jumanne asubuhi tarehe 26.08.2025

Zaburi 37:32-34

32 Mtu asiye haki humvizia mwenye haki, Na kutafuta jinsi ya kumfisha.

33 Bwana hatamwacha mkononi mwake, Wala hatamlaumu atakapohukumiwa.

34 Wewe umngoje Bwana, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Wasio haki watakapoharibiwa utawaona.

Haki huinua Taifa;

Mfalme Daudi anaimba wimbo unaohusu kuishi kwa kutenda haki, maana Bwana ni mwenye haki. Katika mashairi machache tuliyosoma, anasema asiye haki humuua mwenye haki! Yaani Daudi anasema kutokutenda haki kwa njia yoyote kama uuaji ni chukizo kwa Mungu, na yeyote afanyaye hivyo atahukumiwa. Ukisoma nyuma kidogo unamuona Daudi akiimba kuhusu haki;

Zaburi 37:27-30

27 Jiepue na uovu, utende mema, Na kukaa hata milele.
28 Kwa kuwa Bwana hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzao wa wasio haki ataharibiwa.
29 Wenye haki watairithi nchi, Nao watakaa humo milele.
30 Kinywa chake mwenye haki hunena hekima, Na ulimi wake husema hukumu.

Hitimisho la Daudi kwa sehemu ya wimbo ambao tumesoma ni ushauri wa kumgoja Bwana kwa kuishika njia yake. Ahadi ya Mungu ni kumlinda atendaye haki, lakini wasio haki wataharibiwa. Ni wito kwetu sote kuishi kwa kutenda haki kama Bwana anavyotuagiza, maana Haki huinua Taifa. Amina

Jumanne njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

bernardina.nyamichwo@gmail.com