Date:
22-07-2025
Reading:
Wakolosai 2:18-19
Jumanne asubuhi tarehe 22.07.2025
Wakolosai 2:18-19
18 Mtu asiwanyang'anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili;
19 wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu.
Tudumu katika fundisho la Kristo;
Katika sura ya pili, Mtume Paulo anawaandikia watu wa Kanisa la Kolosai juu ya kuishi katika neema ya Yesu Kristo. Anawaandikia kwamba wasidanganywe na maneno ya uongo ambayo yaweza kuwatia katika ushawishi kuwatoa kwa Kristo. Somo la asubuhi ni sehemu ya sura ya pili, ambapo tunaona Paulo akiwasihi watu wa Kolosai kuwa makini ili wasinyang'anywe thawabu yao, yaani wokovu.
Msingi wa ujumbe wa Paulo asubuhi hii ni kukaa katika neema ya Kristo na kuepuka ushawishi ambao unaweza kututoa kwake, sisi kama kundi la waaminio. Kumbe tunakumbushwa kuwa makini katika njia ya ufuasi ili tusije iacha njia ya kweli, yaani Yesu Kristo. Ni kwa kulisoma neno la Mungu na kulishika tunadumu katika fundisho la Kristo. Amina
Jumanne njema
Heri Buberwa