Date:
11-06-2025
Reading:
Yohana 14:25-26
Jumatano asubuhi tarehe 11.06.2025
Yohana 14:25-26
25 Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu.
26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
Roho Mtakatifu ni ushindi wetu;
Ni ujumbe wa Yesu kuhusu ahadi ya Roho Mtakatifu kama anavyoanza kuitoa katika mistari inayotangulia;
Yohana 14:16-18
16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. 18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.Yesu alikuwa anawaandaa wanafunzi ili wakae bila yeye baada ya kuwa ameondoka. Ndiyo maana katika mstari wa 19 anasema "...bado kitambo kidogo hamnioni, bado kitambo mtaniona...". Hapa alikuwa anaongelea kufa na kufufuka kwake, akiwapa ahadi ya Roho Mtakatifu. Ahadi hii hudumu hata sasa, kwamba Roho Mtakatifu ndiye ushindi wetu. Amina
Jumatano njema
Heri Buberwa