Date: 
02-06-2025
Reading: 
Waefeso 6:18-20

Jumatatu asubuhi tarehe 02.06.2025

Waefeso 6:18-20

18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;

19 pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili;

20 ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena.

Mungu husikia maombi yetu;

Mtume Paulo anafundisha juu ya waamini kuvaa silaha za imani (10). Anaandika kwamba kuvaa silaha za Mungu ndiyo zinaweza kusaidia waamini kupinga hila za shetani. Ni kwa mwendelezo huo tunasoma asubuhi hii Paulo akiwahimiza wakristo kufanya sala na maombi kila wakati katika Roho. Katika kuomba huko, Paulo haishii kujiombea tu, lakini kuwaombea wengine. 

Kumbe fundisho la Paulo asubuhi hii ni kuomba wakati wote, tukiomba wenyewe na kuwaombea wengine. Kuomba ni silaha ambayo inatusaidia kupinga hila za shetani. Kupinga hila za shetani maana yake tunaishi kwa kulitii neno la Mungu tukitenda yatupasayo. Inawezekana kupinga hila za shetani kwa kuomba kama tunavyoagizwa, kwa hakikisho la Kristo mwenyewe kusikia maombi yetu. Amina

Uwe na wiki njema

Heri Buberwa Nteboya 

 

0784 968650