Date:
21-05-2025
Reading:
Waefeso 5:18-20
Hii ni Pasaka
Jumatano asubuhi tarehe 21.05.2025
Waefeso 5:18-20
18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;
19 mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;
20 na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;
Kila mwenye pumzi amsifu Bwana;
Mtume Paulo anawaandikia Waefeso kutoenenda katika njia za kipagani, yaani kuenenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Mtume Paulo anawaambia kuacha uasherati, tamaa, maneno ya upuuzi, ubishi, ibada ya sanamu, uongo, na mengine kama hayo. Hayo ni maneno yanayopatikana kwenye mistari kabla ya somo, ambalo sasa linakazia kutolewa kwa mvinyo, bali kujazwa Roho Mtakatifu ili kumpa sifa Mungu na kumshukuru siku zote.
Ujumbe wa Mtume Paulo ni kutenda mambo yote kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu, Mungu mwenyewe. Paulo anasema tukiongozwa na Roho Mtakatifu tunatenda katika Bwana, na sifa zetu zinakuwa kwake. Kwa mujibu wa Paulo, sifa zetu zinakuwa nzuri kwa Bwana tukiongozwa na Roho Mtakatifu kwa sababu tunakuwa tukitenda katika yeye. Roho Mtakatifu awe nasi daima, ili tutumike kwa uaminifu siku zote za maisha yetu. Amina
Jumatano njema
Heri Buberwa