Date:
05-05-2025
Reading:
Isaya 33:21-24
Hii ni Pasaka;
Jumatatu asubuhi tarehe 05.05.2025
Isaya 33:21-24
21 Bali huko Bwana atakuwa pamoja nasi, mwenye adhama; mahali penye mito mipana na vijito, pasipopita mashua na makasia yake; wala hapana merikebu ya vita itakayopita hapo.
22 Kwa maana Bwana ndiye mwamuzi wetu; Bwana ndiye mfanya sheria wetu; Bwana ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa.
23 Kamba zako zimelegea; hawakuweza kukaza sana shina la mlingoti wao; hawakuweza kulikunjua tanga; ndipo mapato ya mateka yaligawanywa, hata wachechemeao walipata mateka.
24 Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.
Yesu ni Mchungaji mwema;
Somo la leo asubuhi ni hakikisho la Bwana kuwa pamoja na watu katika hali yao, wakati wote. Somo linamtaja Bwana kama mwamuzi juu ya watu wake, mfanya sheria na Mwokozi. Ahadi ya Mungu inakazia kuwa hakuna atakayesema kuwa ni mgonjwa, na wote wanaahidiwa kusamehewa uovu.
Ujumbe huu walipewa wana wa Israeli kabla ya kwenda uhamishoni. Pamoja na kwenda uhamishoni, bado Bwana alikuwa upande wao, akiwaahidi kurejea kwenye nchi yao. Ahadi hii hudumu hata sasa, ya kwamba Bwana yuko pamoja nasi daima. Tuzidi kudumu katika yeye, maana yeye ndiye Mchungaji mwema. Amina
Jumatatu njema
Heri Buberwa