Date: 
03-05-2025
Reading: 
Matendo ya Mitume 3:24-26

Hii ni Pasaka

Jumamosi asubuhi tarehe 03.05.2025

Matendo ya Mitume 3:24-26

24 Naam, na manabii wote tangu Samweli na wale waliokuja baada yake, wote walionena, walihubiri habari za siku hizi.

25 Ninyi mmekuwa watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa.

26 Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.

Yesu ajifunua kwetu;

Petro na Yohana wakikwea hekaluni kusali, walimkuta kiwete kwenye mlango wa hekalu ambaye aliwaangalia akitamani kupata kitu kwao. Petro akamwambia kwamba hawana fedha (yeye na Yohana) ila wanampa walichonacho. Akamuombea asimame aende katika jina la Yesu, yule kiwete akatembea.

Watu waliokuwa wakiingia hekaluni walishangazwa na tukio lile. Ndipo Petro akawaeleza habari za wokovu toka enzi za Baba yao Ibrahimu hadi Yesu Kristo ambaye walimkataa na kumsulibisha. Petro aliendelea kuonesha kwamba Yesu huyo ndiye aliyemponya kiwete. Mstari wa 26 ni ujumbe wa Petro, kwamba kwa njia ya Yesu Kristo wangebarikiwa na kuushinda uovu. Yesu anajifunua kwetu akitukumbusha kumcha yeye na kuacha uovu. Amina

Jumamosi njema

 

Heri Buberwa 

 

0784 968650