Date: 
26-04-2025
Reading: 
Mathayo 28:11-15

Hii ni Pasaka

Jumamosi asubuhi tarehe 26.04.2025

Mathayo 28:11-15

11 Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha wakuu wa makuhani habari za mambo yote yaliyotendeka.

12 Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi,

13 wakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala.

14 Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi.

15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo.

Tembea na Yesu mfufuka;

Habari za kufufuka kwa Yesu hazikuwafurahisha waliomsulibisha na kumwua. Baada ya Yesu kufufuka wakapata habari walitahayari, wakafanya vikao na kuchanga hela nyingi ili wawape askari. Askari walielekezwa waseme kuwa wanafunzi wa Yesu walikwenda usiku kaburini wakati askari wamelala wakauiba mwili wa Yesu. Mathayo anasema wapo Wayahudi wanaoamini hivyo hata leo!

Kilichotokea ni aibu kwa waliomkataa Yesu na kumsulibisha, maana ukweli ni kuwa Yesu alifufuka na kuliacha kaburi wazi. Kitendo cha Yesu kufufuka kilitosha kuwaonesha kwamba yule hakuwa mtu wa kawaida kama walivyodhani, kinyume chake waliendelea kuwa na mioyo migumu. Sisi tusiwe na mioyo migumu, tutembee na Yesu mfufuka. Amina

Jumamosi njema

 

Heri Buberwa