Date:
19-04-2025
Reading:
Isaya 52:13-15
Hii ni Kwaresma
Jumamosi asubuhi tarehe 19.04.2025
Isaya 52:13-15
13 Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana.
14 Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake zaidi ya wanadamu),
15 ndivyo atakavyowasitusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu.
Yesu alikufa msalabani kwa ajili yetu;
Isaya alitabiri ujio wa Yesu Kristo, kama Mungu mwenye utukufu aliye na mamlaka juu ya wafalme wote wa dunia. Utabiri wa Isaya haukuishia kwenye ujio tu wa Yesu, bali mateso na kufa kwake kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu. Katika somo, Isaya anamtaja Yesu kama Mfalme ambaye atatukuzwa sana. Ndivyo ilivyotokea, maana alikuja kama Mwokozi, mwenye Utukufu.
Tunapokumbuka Yesu alivyokufa kwa ajili yetu, tufahamu na kuzingatia kuwa atarudi tena. Kwa hiyo tumshike daima, msisitizo ukiwa ni uleule wa kutengeneza njia zetu ili anaporudi asituache, maana yu karibu sasa.
Uwe Jumamosi njema.
Heri Buberwa
Mlutheri