Date: 
04-04-2025
Reading: 
Mwanzo 2:1-4a

Hii ni Kwaresma 

Ijumaa asubuhi tarehe 04.04.2025

Mwanzo 2:1-4a

1 Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.

2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.

3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.

4 Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa.

Tutunze uumbaji (mazingira)

Leo asubuhi tunasoma juu ya uumbaji wa Mungu. Mungu aliumba dunia na vitu vilivyomo kwa siku sita, na somo la leo asubuhi linaonesha siku ya saba akimaliza hiyo kazi ya uumbaji na kustarehe. Tunaona Mungu akiibariki siku ya saba na kuitakasa, kwa sababu ni katika siku hiyo alistarehe. Jambo la muhimu hapa ni kuwa Mungu ndiye aliyeziumba mbingu na dunia.

Ukisoma kuanzia mstari wa saba, unaona Mungu akiumba mwanadamu, anampa na msaidizi. Maana yake ni kuwa Mungu ndiye aliyeumba dunia, sisi wanadamu na vitu vyote vilivyomo. Tunakumbushwa kuwa dunia na sisi ni uumbaji wa Mungu, na tunawajibika kuutunza uumbaji huu ili dunia iendelee kuwa salama kwa viumbe vyote. Amina

Ijumaa njema

Heri Buberwa