Date: 
02-04-2025
Reading: 
Mwanzo 1:1-5

Hii ni Kwaresma 

Jumatano asubuhi tarehe 02.04.2025

Mwanzo 1:1-5

[1]Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

[2]Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

[3]Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.

[4]Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.

[5]Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.

Tutunze uumbaji (mazingira)

Asubuhi hii tunaisoma historia ya uumbaji, mwanzoni kabisa. Tunaona Mungu akiumba mbingu na nchi. Tunaona pia Roho wa Mungu akitulia juu ya vilindi vya maji. Huu ni uthibitisho wa Mungu muumbaji. Alianza kuumba dunia, akamuumba mwanadamu, na vingine vyote. Mungu alitutengenezea sehemu nzuri ya kuishi, yaani dunia tuliyomo. Ameipa uzuri dunia ili tuifurahie.

Uumbaji wa Mungu ni alama ya Upendo kwetu. Ndio maana baada ya uumbaji, hakutuacha, akamtuma Yesu Kristo kufa msalabani, lakini pia akatupa Roho Mtakatifu kwa utakaso. Hivyo asili ya Mungu ni upendo. Tunafanya nini kwa Mungu wetu aliyetuumba, na kutuletea wokovu? Tumwamini, tumpokee, tumfuate, na kumtii ili mwisho wetu uwe mwema. Lakini pia tutunze uumbaji kama anavyotuagiza. Amina

Jumatano njema 

Heri Buberwa