Hii ni Kwaresma
Jumamosi asubuhi tarehe 08.03.2025
Marko 14:32-42
32 Kisha wakaja mpaka bustani iitwayo Gethsemane; akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa muda niombapo.
33 Akamtwaa Petro na Yakobo na Yohana pamoja naye, akaanza kufadhaika sana na kuhangaika.
34 Akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa mkeshe.
35 Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akiomba ya kuwa, ikiwezekana, saa hiyo imwepuke.
36 Akasema, Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.
37 Akaja akawakuta wamelala usingizi, akamwambia Petro, Je! Simoni, umelala? Hukuweza kukesha saa moja?
38 Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu.
39 Akaenda zake tena, akaomba, akisema neno lilo hilo.
40 Akaja tena akawakuta wamelala, maana macho yao yamekuwa mazito, wala hawakujua la kumjibu.
41 Akaja mara ya tatu, akawaambia, Laleni sasa, mpumzike; yatosha, saa imekuja; tazama, Mwana wa Adamu anatiwa mikononi mwao wenye dhambi.
42 Ondokeni, twendeni zetu; tazama, yule anayenisaliti amekaribia.
Tutubu na kumrudia Mungu;
Yesu alikuwa anakaribia kusalitiwa, ambapo asubuhi hii tunasoma akiwa kwenye bustani ya Gethsemane akiomba. Alikuwa na Petro, Yakobo na Yohana, akawaambia wakeshe naye. Ilikuwa ni wakati wa kufadhaika, ni wakati alipoomba kikombe kimuepuke, lakini kwa mapenzi ya Mungu. Mwili ulikuwa dhaifu, lakini roho ilikuwa radhi! Msisitizo wake ulikuwa kwa wanafunzi kukesha alipokuta wamelala.
Tunachosoma ni hatua wakati Yesu anaelekea Kalvari. Haikuwa safari nyepesi. Yesu alikuwa Mungu kweli na mwanadamu kweli. Kama mwanadamu, alifikia mahali akaomba kikombe kimuepuke! Ombi lake halikujibiwa lakini alikufa akiwa katika uhusiano mzuri na baba yake. Alipokea jibu lake kwa kufa. Tukeshe na Yesu, yaani tumwamini daima, ili kwa njia ya kifo chake tuurithi uzima wa milele. Amina
Jumamosi njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650