Date: 
27-02-2025
Reading: 
Waefeso 6:10-17

Alhamisi asubuhi tarehe 27.02.2025

Waefeso 6:10-17

10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.

11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.

12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,

15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;

16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;

Neno la Mungu ni silaha imara;

Mtume Paulo anawaandikia watu wa Kanisa la Efeso kuwa hodari katika Bwana. Anawataka kuvaa silaha za Mungu ili waweze kuzipinga hila za shetani. Paulo anaonesha kuwa kushindana na mwovu siyo rahisi, ndiyo maana anawaambia kusimama imara katika Bwana. Msisitizo wa Paulo ni kuwa vita ya imani siyo ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya.

Hitimisho la somo ni Paulo anaposema kuwa chapeo ya wokovu na upanga wa Roho ni neno la Mungu. Hivyo Paulo anawasihi watu wa Efeso kuishi kwa neno la Mungu ili kumshinda mwovu shetani. Nasi tunakumbushwa kuishi kwa neno la Mungu ili tumshinde mwovu shetani. Amina

Alhamisi njema

Heri Buberwa