Date:
14-02-2025
Reading:
Yohana 3:33-36
Hii ni Epifania
Ijumaa asubuhi tarehe 14.02.2025
Yohana 3:33-36
33 Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri ya kwamba Mungu ni kweli.
34 Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.
35 Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake.
36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Utukufu wa Mwana wa Mungu;
Yohana anaandika juu ya Yesu Kristo atokaye mbinguni. Yohana anasema Kristo hunena neno la Mungu maana ametoka kwa Mungu. Na mimi naongezea, ni Mungu kweli. Yohana anaendelea kusema kila amwaminiye anao uzima wa milele, na asiyemwamini hatauona huo uzima, bali ghadhabu ya Mungu.
Ukisoma nyuma kidogo unaona Yohana anavyomtambulisha Yesu atokaye mbinguni;
Yohana 3:31-32
31 Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote. 32 Yale aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoyashuhudia, wala hakuna anayeukubali ushuhuda wake.Yohana alikuwa anamuelezea Yesu ambaye Wayahudi walimkataa. Lakini Yohana anakazia kwamba alitoka mbinguni, yuko juu ya vyote. Huyu ndiye atarudi tena kulichukua Kanisa. Tumwamini ili tuurithi uzima wa milele. Amina
Ijumaa njema
Heri Buberwa
Mlutheri