Hii ni Epifania
Alhamisi asubuhi tarehe 13.02.2025
Ezekieli 12:21-25
21 Neno la Bwana likanijia, kusema,
22 Mwanadamu, ni mithali gani hii mliyo nayo katika nchi ya Israeli, mkisema, Siku hizo zinakawia na maono yote hayatimizwi.
23 Basi uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Nitaikomesha mithali hii, wasiitumie tena kama mithali katika Israeli; lakini uwaambie, Siku hizo ni karibu, na utimilizo wa maono yote.
24 Kwa maana hayatakuwapo tena maono yo yote ya ubatili, wala ubashiri wa kujipendekeza, katika nyumba ya Israeli.
25 Maana mimi ni Bwana; mimi nitanena, na neno lile nitakalolinena litatimizwa; wala halitakawilishwa tena; maana katika siku zenu, Ewe nyumba iliyoasi, nitalinena neno hilo na kulitimiza, asema Bwana MUNGU.
Utukufu wa Mwana wa Mungu;
Tunasoma unabii wa Ezekieli kwamba hukumu ya Mungu ipo, haitahairishwa. Israeli waliona siku za kuishi ni nyingi, hivyo habari za hukumu hazikuwa na uhalisia. Bwana anamwambia Ezekieli kuwaambia Israeli kuwa ataikomesha mithali hii, maana yake kuwa mawazo yao hayakuwa ya kweli, bali hukumu itakuwepo.
Ezekieli anaendelea kusema kuwa mawazo ambayo yako kinyume na Bwana ni ubatili. Ezekieli aliwataka watu kuishi kama Bwana alivyowaita, na siyo walivyotaka ili kuiepuka hukumu. Hata sasa, Yesu hutuita tumpokee na kuishi kwa njia ya neno lake ili tuwe na mwisho mwema katika yeye. Amina
Alhamisi njema
Heri Buberwa