MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 26 JANUARI, 2025  

SIKU YA BWANA YA 3 KATIKA MAJIRA YA UFUNUO

NENO LINALOTUONGOZA NI  

MUNGU HANA UPENDELEO

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia kwa cheti: 

3. Matoleo ya Tarehe 19/01/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 12/01/2025 ilikuwa ni washarika 810. 

6. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

7. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=. 

8. SHUKRANI: TAREHE 02.02.2025 KATIKA IBADA YA KWANZA SAA 1.00 ASUBUHI

  • Jumuiya ya Upanga itamtolea Mungu shukrani ya pekee kwa matendo makuu Mungu aliyowatendea.

Neno: Yeremia. 10:6, Wimbo: TMW 166(Wamwendea Yesu) 

IBADA YA TATU SAA 4.30 ASUBUHI

  • Familia ya Bwana na Bibi Theophilus Mlaki pamoja na familia ya Marehemu Mama Caroline Kweka. Watamtolea Mungu shukrani kwa kuwalinda muda wote tangu Mama yao Mpendwa Caroline Kweka alipotwaliwa na Bwana miaka kumi iliyopita, Mama yao Caroline alikuwa akiwaombea sana katika uhai wake.

Neno: Zab. 138:1-3, Wimbo: TMW 405 

9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo 
  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Zimba 
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mujuni Mutembei
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi David Mollel
  • Mjini kati: Watafanyia hapa kanisani saa 1.00 asubuhi.
  • Mikocheni, Kawe na Mbezi Beach: kwa Bwana na Bibi Freeman Mbowe.

10. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la pili  

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo

yetu, Bwana ayabariki.